Saturday 20 February 2016

THOMAS ULIMWENGU TISHIO MAZEMBE



TP Mazembe imechukua kwa mara ya tatu African Super Cup baada ya kuifunga Tunisian Red Devils “Etoile Du Sahel” kwa magoli 2-1. TP Mazembe imepata ushindi kutokana na magoli ya striker wa Ghana Daniel Nii Adjei ambae alitupia goli la kwanza dakika ya 20 na 45.Mechi hiyo iliisha kwa kushuhudia goli moja la pekee kwa upande wa Etoile Du Sahel kutoka kwa Mohamed Msekh.
Mtanzania Thomas Ulimwengu amekua mchezaji kwanza kutoka Tanzania kushinda kombe hili baada ya mechi ya leo.
Thomas aliingia dakika ya 73, kwa mujibu wa taarifa ni kwamba kocha hakuweza kumchezesha muda mrefu kwasababu ana maumivu ya kifundo cha mguu alipata kwenye mechi dhidi ya Lupopo. Kuna uwezekano akapewa wiki nzima kupumzika ili apone vizuri

NGASA SI KITU KWA MADIBA


MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa (pichani juu) amecheza dakika zote 90 timu yake, Free State Stars ikichapwa mabao 2-0 na Chippa United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Absa Afruka Kusini Uwanja wa Nelson Mandela Bay mjini Port Elizabeth leo.
'Chilli Boys' wanabaki nafasi ya sita katika msimamo wa ligi pamoja na ushindi huo, huku Ea Lla Koto wakiporomoka hadi nafasi ya nane.
Mabao ya Chippa yamefungwa na Xola Mlambo dakika tatu kabla ya mapumziko na Nkosinathi Mthiyane dakika ya 72.

Kikosi cha Chippa kilikuwa: Akpeyi, Mthiyane/Zuke dk90, Okwuosa, Macheke, Thopola, Chipeta, Mlambo, Sangweni, Bance/R. Manzini dk65, Zulu/Sali dk43 na Molangoane.
Free State Stars: Diakite, Masehe, Mashego, Sankara/Venter dk74, Chabalala, Kerspuy, Thebakang/Gopane dk11, Jaftha/Nkosi dk45, Thethani, Ngassa na Vilakazi

simba chali:yanga hai hai


Image result for hamisi tambwe  Image result for mashabiki wa yanga

hatimaye  young afrikan yonesha ubabe baada ya kuichapa simba sport club bao mbili kwa bila katika mchezo uliopigwa leo katika uwanja wa taifa jijini dar es salaam na  kuandika rekodi ya kuwachapa wapinzani wao hao bao 2-0 mfululizo katika ligi ya vodacom tanzania bara mwaka 2015/2016